Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, March 24, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tisa ( 39 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Olvia alizungumza huku akiwa amemshika mtoto mchanga ambaye sikuweza kumuona vizuri sura yake.Olvia Hitler akanyoosha mkono wake kwenye  moja ya lango kubwa,ukafunguka na yakatoka majitu mawili yakutisha yakiwa na vishoka vikubwa na kuwafanya watu waliopo hapa kuanza kushangilia

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nikiyatazama majamaa yanayo kuja kwa mwendo wa taratibu ulio jaa vishindo.Nikatazama vishoka walivyo vishika na kujikuta mwili mzima ukiingiwa na hufu

“NIMERUDI”
Nikaisikia sauti ambayo mara kwa mara huwa inanielekeza nini cha kufanya,
“Muda wote ulikuwa wapi hadi umeniacha nimekuja huku chini?”
“NILIKUWA NINAMANA YANGU”
“Maana gani?”
“MANAA KUU NI KWAMBA UJE KUICHUKUA DAMU YAKO KABLA HAWAJAKUDHURU ZAIDI”
“Sasa nitamchukuaje?”
“USIJALI KWA HILO”
Sauti ninayo zungumza nayo kidogo ikanipa matumaini ya kuweza huku kizimu nilipo.Nikastukia  kuona watu watu wapatao sita,walio valia mavazi meupe wakiwa wamenizunguka.Mwanga mkali mweupe ukaanza kumulika katika eneo zima lililo kaa watu wanaoshangulia.Mwanga ukasababisha miili ya watu hao kuanza kupasuka vipande vipande.Majiu yaliyokuwa yakinifwata nayo yakaanza kupasuka vipande vipande.Olvia Hitler akabaki akiwa amenitazama kwa macho makali.Sikuweza kujua ni kwanini mwanga haukuweza kumdhuru,
“Mbona yule msichana audhuriki na huu mwanga”
“TUNAUA KWANZA WATU WAKE”
Watu walio nizunguka,wakaanza kazi ya kukimbia huku wakinizunguka kwa kasi kubwa,Nikajashangaa nikianza kupanda kwenda juu hadi nikafika sehemu alopo Olvia Hitler,
“USIMUOGOPE MSOGELEE”

Nikaanza kupiga hata za taratibu huku nikiwa ninajiamini sana,Olvia Hitler akabaki akinitazama kwa macho makila
“MCHUKUE HUYO MTOTO,HAWEZI KUKUZUIA TUMEMFUNGA MWILI WAKE”
Nikaupeleka mkono wangu wa kulia alipo mtoto,Olvia hakuweza kunifanya kitu chohote zaidi ya kubaki akinishanga,Nikamchukua mtoto wangu,Jambo ambalo linaniogopesha juu ya huyu mtoto ni jinsi alivyo.Sura yake haijaendana kabisa na mimi hata mwili wake si wakawaida kama watoto wengine
“Hivi huyu ni mwanangu kweli?”
“WEWE MCHUKUE HUYO MTOTO TUONDOKE”
Sikuwa na lakuuliza zaidi ya kumchukua mtoto,Nikajistukia nikivutwa nyuma,watu walio nizingira kwakanishika na kuanza kwenda juu.Tukiwa katikati kuna sehemu nikaiona ikiwa na moto mwingi sana
“Pale ni wapi?”
“NI KWENYE ZIWA LA MOTO,WALE WOTE AMBAO WANAFANYA MAOVU WANAPELEKWA KULE.NA SIKU YA MWISHO WA DUNIA MOTO UTAONGEZEKA MARA DUFU”
“Mmmmm naweza kwenda kupaona?”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )