Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, March 5, 2018

TRC yakitolea maelezo kichwa cha treni kilichopata ajali

Shirika la Reli Tanzania (TRC), limekanusha kwamba kichwa cha treni kilichopata ajali mwishoni mwa wiki ni miongoni mwa vilivyotelekezwa bandarini ambavyo vilikutwa havina mwenyewe na Rais Magufuli.

Ofisa uhusiano wa shirika hilo, Mohammed Mapondela alisema jana kwamba taarifa hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli.

Katika ajali hiyo, watu 21 walijeruhiwa baada ya treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Tabora kuelekea Kigoma kupata ajali eneo la Malagarasi wilayani Uvinza.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema kwamba ajali hiyo ilitokea Februari 27 saa nane mchana.

Katika ajali hiyo, kichwa cha treni kiliacha njia na kuanguka pamoja na mabehewa mawili.

Akifafanua kuhusu kichwa hicho Mpondela alisema, “Watu wanashindwa kuelewa kuwa kichwa kilichopata ajali ni 9001 ambavyo ni vya awamu ya kwanza, hivi vilivyopo bandarini pamoja na kwamba Serikali imeshavinunua bado havijaanza kutumika.”

Kuhusu ripoti ya ajali hiyo alisema bado haijatoka na kwamba wataalamu wanaendelea na uchunguzi. 

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )