Tuesday, March 13, 2018

Viongozi CHADEMA Waripoti Tena Polisi

Viongozi wa Chadema waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi leo Jumanne Machi 13, 2018 wametakiwa kufika tena kituoni hapo Machi 16, 2018.

Licha ya kutakiwa kuripoti viongozi saba, waliofanikiwa kufika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.

Viongozi wengine watano akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshindwa kuripoti kutokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vilivyoanza leo mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, wametakiwa kuripoti Machi 16, saa 2:00 asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho Dk Mashinji amesema, “Viongozi wote wameshatoa maelezo yao. Leo tumeripoti wawili na viongozi wengine ni wabunge na wapo Dodoma walishindwa kujigawa katika mambo mawili.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )