Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, March 25, 2018

Wajasiriamali Wanawake 600 Wapata Mikopo Isiyo na Riba

Na Ferdinand Shayo,arusha.
Serikali mkoani Arusha kwa kushirikiana na wafanyabiashara, wametoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya milioni 120 Kwa wajasiriamali wadogo wanawake 600 hatua ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Waziriwa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Walemavu  Jenister Muhagama, akikabidhi mikopo hiyo jana jijini Arusha alisema serikali itaendelea kuwakwamua wanawake kiuchumi, hii inatokana na asilimia kubwa ya utafiti kuonyesha wanawake ndio wengi wanakabiliwa na changamoto zakutokuwa na ajira .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa huo ni mwendelezo wakuwasidia wananchi wa hali ya chini wasiokopesheka na benki kutokana na uwepo wamasharti magumu hivyo mkopo huo utawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo Marrygoreth Leonard alisema itawainua kutoka hatua moja hadi nyinge na kujikwamua kiuchumi,

Wadau waliofanikisha mikopo hiyo akiwemo Mfanyabiashara Willbard Chambulo,  waliahidi kuendelea kuwasaidia wanawake hao ili kupunguza umasikini katika kaya nyingi za wakazi wa jiji la Arusha.

Mikopo hiyo ni sehemu ya marejesho ya zaidi ya milioni mia tatu zilizotolewa kwa waendelesha bodaboda katika mkoa wa Arusha ambazo wameshazirejesha.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )