Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, March 7, 2018

Watanzania 225 Huambukizwa Virusi Vya Ukimwi Kwa Siku

adv1
Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa Virusi vya Ukimwi kwa siku.

Hali hiyo inamaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni 81,000.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, jana  Jumanne Machi 6, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi.

Alisema hali hiyo ni mbaya zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

“Asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

“Hii inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake,” alisema Dk. Maboko.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )