Wednesday, March 21, 2018

Watuhumiwa Wawili Wa Ujambazi Wauawa Wakijibizana Risasi Na Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.

Pia limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani Kasulu.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema ilipofika majira ya saa 5:00 usiku  wa Machi 19, 2018 kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.

Amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata.
 
"Baada ya kuhojiwa na polisi waliwataja wenzao na kufanikiwa kuwakamata wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio ya mauaji  na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

"Hata hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu,"amesema.

Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.

Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo watanzaa msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )