Sunday, March 4, 2018

Wawili Watupwa jela kwa 'kumchezea rafu' Rais Nkurunziza katika mechi ya kirafiki

Maofisa wawili nchini Burundi wamehukumiwa kwenda jela baada ya Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kuwashutumu ‘kuchezewa vibaya’ wakati wa mechi ya mpira wa miguu waliyoiandaa.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye ni 'Mlokole' wa Kanisa la Evangelical Christian amekuwa akitumia muda wake mwingi kusafiri na Timu yake ya Haleluya FC ndani ya Burundi kwa ajili ya kushiriki mechi mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Februari 3, Rais huyu na timu yake walicheza na Timu ya mji wa Kaskazini mwa Kiremba.

Kama kawaida, upande wa timu pinzani ulikuwa ukifahamu kuwa unacheza na rais wa nchi na kukubaliana kuwa mchezo utakaochezwa utakuwa mwepesi, na hata kuweza kumruhusu Nkurunziza kufunga goli.

Lakini kutokana na Timu ya Kiremba kuwa na wachezaji wengi ambao ni wakimbizi kutoka Congo ambao hawakujua kama wanacheza na rais wa Burundi, walikuwa “wakimshambulia mara kwa mara anapokuwa na mpira na kumwangusha mara kadhaa", shuhuda aliwaeleza AFP.

Waliohukumiwa kwenda jela, Juzi Alhamisi ni pamoja na Mratibu wa Kiremba Cyriaque Nkezabahizi na msaidizi wake, Michel Mutama, kwa mujibu wa shirika la habari.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )