Sunday, March 25, 2018

Waziri Kalemani Aipa TANESCO Miezi Mitatu Ianze Kununua Mita za Luku za Wazalishaji wa Ndani

Waziri wa Nishati, Dk Merdard Kalemani amesema Serikali itafanya tathmini ya mahitaji ya mita za luku kabla ya kupiga marufuku uagizaji mita hizo kutoka nje ya nchi.

Amesema tathmini hiyo itafanyika kwa siku 90 kuanzia jana Jumamosi Machi 24, 2018 baada ya hapo hakutakuwa na uagizaji wa mita hizo kutoka nje kutokana na uzalishaji ulioanza kupitia viwanda vya ndani.

Ametoa kauli hiyo jana  Machi 24, 2018 wakati wa ziara katika kiwanda cha kutengeneza mita za umeme wa luku cha Baobab Energy System Tanzania (Best).

Kiwanda hicho kimeanza kutengeneza mita za aina hiyo Machi 15, 2018 kikianza na uzalishaji wa wastani wa mita hizo 1000 kwa siku zinazotumika kwa wateja wa kawaida.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )