Thursday, March 29, 2018

Serikali Yawasamehe Roma Mkatoliki na PretyKind, Wafutiwa Adhabu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza, leo wametangaza kufuta adhabu ya kufungia wasanii wa  muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki na Suzan Michael maarufu kama Pretykind.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki ambaye naye aliongozana na Waziri Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa kibamia ataviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo.

Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongezi kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )