Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, March 13, 2018

Zari: Natafuta Pesa, Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya

adv1
Zari ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.

Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.

Kupitia kurasa yake ya SnapChat  Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema; “Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada  wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya ni kwa ajili ya mwanaume mpya”.

Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:

"Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )