Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, April 9, 2018

Agness Masogange: Sitaki Mazoea na Mtu

Videi vixen maarufu Agnes Gerald maarufu kama Masogange amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hataki kabisa masuala ya shobo na watu baada ya kesi yake badala yake anataka kuwa kivyake.

Wiki iliyopita Masogange aliponea chupu chupu kwenda jela baada ya kuhukumiwa miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 ambayo alifanikiwa kuilipa na kuepuka jela.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Masogange alisema kuwa, kwa sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.

 "Sasa hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida kabisa“.

Agnes alikamatwa mwaka jana Kwa Tuhuma za kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na mkemia mkuu wa serikali alithibitisha hayo baada ya kumpima.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )