Thursday, April 5, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 77 na 78 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
ILIPOISHIA  
  Nilimuamrisha jamaa huyu, ila akaonekana haielewi lugha ninayo izungumza. Ahmood akabaki amekodoa macho, kwa nguvu nikamshika shingo jamaa huyu na kumuinamisha na kumfanya abong’oe na kuyaacha makalio yake yaeleke kwa Ahmood.
“Ahmood vuo nguo zako na wewe uwafanye kama kile walicho kifanya wewe”
Maneno yangu yakazidi kumshangaza kwani hakutegemea kabisa kama ninaweza kulifanya tukio hilo. Nikakazia macho Ahmood ambaye naye kwa woga akaanza kuvua suruali yake haraka haraka ili kufanya kile ambacho ninamuambia akifanye.
      
ENDELEA  
Ahmood akamalizia kuvua suruali yake pamoja na nguo yake ya ndani, nikabaki nimeshangaa kwani, umme wake ni mdogo sana kama kidole changu cha mkono tena cha mwisho. Japo umesimama ila sikujua hata hili zoezi atalifanya vipi.
Sikuwa na jambo la kuzungumza kwa maana Mungu amemuumba kila mwanaume na maumbile yake, wapo wenye maumbile makubwa wapo wenye maumbili ya saizi ya kati na wapo wenye maumbile madogo kama mwenzangu Ahmood.
“No, Dany siwezi kufanya hivi”
Ahmood alizungumza huku akitetemeka, anaonekena amefwata amri yangu ya kuvua nguo ila sio mapenzi yake kutoka moyoni. Sikuwa na la kufanya zaidi ya kumuachia jamaa wa watu ambaye muda wote hakuweza kukurupuka kutoka mikononi mwangu kwa maana nilimkaba kisawa sawa.

Ahmood akapandisha suruali yake taratibu huku akinitazama kwa macho ya woga, sikuhitaji kuiweka sura yangu katika muonekano wa hasira. Nilipo hakikisha amemaliza kuvaa, taratibu tukaondoka huku jamaa tukimuacha katika hali ya wasiwasi mkubwa sana. Hatukuzungumza kitu cha ina yoyote. Tukiwa njiani nikakutana na askari aliye niita kwa namba yangu na kuniomba niongozane naye. Nikamfwata nyuma nyuma hadi kwenye moja ya chumba ambacho kimejaa magunia mengi. Akatoka na kuufunga mlango kwa nje nikabaki peke yangu nikishanga shangaa.
  
Wakatokea manjemba manne yaliyo shiba nyuma ya magunia haya yaliyo pangwa vizuri kwenda juu. Manjemba haya kila mmoja mkononi mwake amasika fimbo aina ya mkia wa taa. Kila njemba ambalo ninaliangalia halionyeshi sura ya huruma wala kuhofia chochote kutoka kwangu.

“MUNGU NISAIDIE”  
Nilizungumza maneno hayo huku nikirudi rudi nyuma kwa maana majama haya, miili yao imekatika kisawa sawa, miili yao imevimbiana kwa misuli minene. Taratibu ikaanza kugawanyika, ikijaribu kunizunguka, uzuri haya magunia yamekaa katika mfumo wa ngazi ambao mtu unaweza kupanda kiurahisi pasipo kupata shida ya aina yoyote. Njemba hizi ambazo ninaamini kwamba wametumwa kunishuhulikia kutokana nimevamia gereza kwa ubabe, ikaanza kurusha mikia yao ya taa, kwa kadri ya uwezo wangu nikajitahidi kuhakikisha kwamba ninaikwepa kwa kila namna huku nikizidi kupanda juu ya magunia haya.

Uzuri wa wangu ni wepesi wa kuweza kuruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ila hii mijamaa ni mizito sana, udhaifu wao ukawa ndio silaha yangu kubwa kwangu kwani kila walipo jaribu kuruka nilijitega kuhakikisha kwamba ninamrudisha alipo toka kwa teka ama kwa kumsukuma. Ikawa ni mchezo wa kukimbizana huku nikiendelea kuikwepa fimbo zao za mikia ya taa.

Karibia lisaa zima kazi yangu ikawa ni kukwepa na kupanda juu ya magunia, udhaifu ukajitokeza tena kwa hizi njemba, kwani wote ikafikia hatua wakachoka kukimbizana na mimi na ikawa ni rahisi kwangu kuanza kuwashambulia kwa kuwasukumia magunia haya mazito yaliyo jaa vyakula vya wafungwa. 

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )