Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, April 6, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 79 na 80 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-                              
ILIPOISHIA 

Hata kabla Vivia hajanijubu chochote, mlango huu ukaanguka chini baada ya kuvunjwa kwa nguvu. Kundi kubwa la wasichana hawa wakijeshi wakiwa wameongozana na mkuu wao wa hili gereza wakasimama mlangoni, huku nyuso ya huyu mwana mama mkuu wao ikiwa imetengeneza alama ya ‘V’ kutokana na hasira kali aliyo nayo. Vivian na wezake wakajikuta wakikurupuka kila mmoja akajawa na wasiwasi mwingi sana kwani kinacho kwenda kutokea Ahmood alisha wahi kuniambia.

ENDLEA      
Mama huyo akawaamuru wanajeshi wengine kuwakamata wezao ambao wote wapo uchi, haya mimi mwenyewe nipo kama nilivyo zaliwa. Vivian alipo karibiwa kukamatwa na mwenzake mmoja, akaanzisha varangati, jambo lililo nipa hata mimi nguvu. Wezake wengine nao watatu kazi ikawa ni kupambana na hawa wanajeshi wezao.
Japo tupo uchi wa mnyama wala hatukulijali hilo, kikubwa hapa ni kila mtu kuyaokoa maisha yake. Hapa ndipo nilipo gundua kwamba wasichana hawa mapigano yao hayana tofauti kabisa na wasichana wa Livna.
  
Vivian hakuwa mbali na mimi, kila msichana ambaye alihisi anaweza kunizidi aliweza kumdhibiti kisawa sawa. Tulipo pata upenyo wakutoka katiki hichi chumba kilicho jaa damu nyingi, tukatoka na kuanza kukimbia hivyo hivyo tulivyo. Vivian akawa na kazi ya kuniamrisha nimfwate nyuma. Kutokana taa zimewashwa na ving’ora vimepigwa kila sehemu, haikuwa rahisi kwetu sisi kuto kuona tunapo elekea. Tukaingia kwenye moja ya chumba ambacho ni cha kuhifadhia nguo za wanajeshi hawa.

“Chagua haraka haraka nguo itakayo kutosha”
“Poa”
Nikaanza kuchambua suruali ambazo zinaweza kunienea, kwa habatiu nzuri sikupata shida kabisa, nikapata moja ya suruali ambayo imeniendelea vizuri. Nikaikavaa na kufunga zipu  pamoja na vifungo chake, nikatafuta na shati la juu ambalo nalo pia ni la kijeshi, nikavaa.
“Chukua viatu hivyo”  
Vivian alinirushia buti za kijeshi huku akiwa anamalizia na yeye kuvaa.
“Hivi unafahamu njia ya kutokea humu ndani?”  
“Yaaa ninaifahamu ila ni ya hatari kubwa sana, ni heri kwenda kufia huko mbele ya safari kuliko kukamatwa na huyu jinni. Kifo chake ni kibaya sana”

“Mmmmm”
“Tuondoke”
Vivian alizungumza huku akiusogelea mlango, akausukuma taratibu na kuchungulia nje, sikujua ameona kitu gani, kwa ishara akaniomba nirudi nyuma, tukajificha kwenye moja ya kabati kubwa. Wakaingia wasichana wawili wakiwa na silaha, wakaanza kuchunguza taratibu ndani ya hichi chumba. Vivian akanipa ishara ya kwamba kila mmoja apambane na wakwake. Ndivyo ilivyo kuwa pale wasichana hawa walivyo jaribu kulisogelea kabati tulilo jificha, kilicho wakuta, mi Mungu tu ndio anaye jua, kwa maana kila mmoja alimuua wa kwake kwa staili anayo ijua yeye. Tukazidi kujiamini sana baada ya kuzipata bunduki zao, Vivian akakimbilia mlangoni akachungulia nje kwa mara nyingine, kwa ishara akaniita hadi mlangoni na tukatoka na kuanza kukimbilia nje.

“Tupite huku”
Vivian alizungumza huku akikunja kushoto, tukazidi kusonga mbele kwenye njia ambazo ndio mara yangu ya kwanza kuziona ndani ya hili gereza.
“Dany kuwa makini huku tunapo pita ni njia ambayo kunafugwa majoka makubwa sana na tusipo kuwa makini tutafia huko”
Vivian alizungumza huku jasho jingi likimwagika usoni mwake, nikajikuta nikishusha pumzi kusema kweli, mbele ya majoka haya hakuna mtu ambaye anaweza kuwa jasiri kwa maana majoka hayo anayo yazungumza Vivian sijui hata yanafananiaje.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )