Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 14, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 85 na 86 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-                       
ILIPOISHIA   

Tulipo  hakikisha wanajeshi tumewadhibiti na kuwaua wote nata maderava wa magari haya tukaalisogelea gari moja na kulifungua kwenye moja ya kontena. Tukakuta shehena kubwa ya chakula ikiwa impengwa vizuri kwa mfumo wa vigunia.  Tukiwa katika kutazama chakula kilichopo kwenye makontena haya, kwa mbali tukasikia milio ya helicopter za jeshi.  Haikupita hata dakika mbili, helicopter mbili zikawa zimefika aneo la tukio na tukaanza kushambuliwa kutokea juu, jambo ambalo likaanza kutupa wakati mguu sana na kumchanganya kila mmoja aliyopo katika hili eneo hususani Hawa ambaye alisha anza kusherekea ushindi wa chakula hichi kingi kupita hata kilicho teketea kwenye ghala la chakula.

ENDELEA  
Sote tukajibanza kwenye magari haya kwa maana mtu usipo kuwa makini unaweza kujikuta unapoteza maisha. Hawa akatoa ishara nikamuona msichana mmoja akitambaa chini ya magari haya hadi kwenye moja yagari letu tulilo jia. Akachukua bomu moja la kutungulia helcopter, akapiga goti moja chini huku mwengine akiwa amelikunja, kisha akailiweka bomu hilo juu ya bega leke. Akaipima moja ya halcopter, kisha akaliachia bomu hilo ambalo, halikukosea kuelekea kwenye helcopter ambayo lilitumwa.

Helcopter hiyo ya wanajeshi wa umoja wa mataifa akalipuka, na kubaki moja. Msichana huo mwenye nguvu kama za kike akachukua bomu jengine na kukaa mkao kama alio kuwa amekaa hapo awali, akafyatua bomu hilo na kuipiga helcopter ya pili, iliyo anza kuzunguka kwa kasi hewani huku ikiwaka motona kuanguka chini.
Baada ya shambulizi hilo, sote tukatoka chini ya magari huku tukiwa tunashangilia. Tuakingia kwenye magari haya, na kuanza safari ya kuelekeea kwenye ngome yetu. Gari ninalo liendesha, lipo nyuma ya kabisa. Huku nyuma yangu kukiwa na gari ndogo moja tuliyo kuja nayo. Safari yetu ikachukua zaidi ya lisaa, tukaw tumesha fika katika ngome yetu. Tukayaingiaza magari hayo yote kwenye ngome yetu, na ulinzi ukazidi kuimarishwa.
“Mkuu kuna taarifa”
Kijana mmoja alizungumza kwa lugha ya kiarabu huku akimtazama Hawa machoni, na mimi nilipo jaribu kuyakutanisha macho yetu na kijana huyo akaonekana kuyakwepesha. Kutokana sikuwa na haja kufwatilia ni taarifa gani ambayo inayo endelea, ikanibidi kuondoka katika eneo hili kueleka katika chumba ambacho tunahifadhia silaha nzito.
Kabla sijatoka katika chumba hichi, wakaingia jamaa wawili wakasimama nyuma yangu.
“Dany upo chini ya ulinzi”
“Chini ya ulinzi!!?”

“Ndio”
“Kwa kosa gani?”
“Utakifahamu tu, ukiwa katika chumba cha ulinzi”
Kutokana walio agizwa kunikamata ni afiki zangu, sikuhitaji kufanya fujo yoyote. Nikakubali kuvishwa pingu ya mikononi na nikaongozana nao hadi kwenye chumba maalumu cha mahojiano, ambacho kimefungwa kameza kama sita na kina Tv kubwa inayo onyesha pembe zote za kila kamera ndani ya hichi chumba.
Akaingia moja ya kiongozi ambaye kwa siku zote ambazo huwa nina msalimia hakuwahi kuipokea salamu yangu. Akanitazama kwa macho makali huku akikuna kuna ndevu zake ndefu kama za Osama Bin Laden.
“Asalam alyakum”
Alinisalimia huku akikaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu na tumetenganishwa na meza ya chuma katikati yetu.
“Salama”
“Wewe ni nani?”
Swali lake likaanza kunistua akilini mwangu, ila nikajifanya kama sio mtu ambaye ninajijua mimi ni nani.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )