Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, April 11, 2018

Asilimia 5.8 ya Watanzania ni walemavu

Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu 2,641,802 sawa na asilimia 5.8 ya wananchi wote.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa ameliambia Bunge leo Jumatano Aprili 11, 2018  kuwa idadi hiyo inabainishwa kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambayo ilijumuisha vipengele vya kuwatambua wenye ulemavu.

Amesema ulemavu umegawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wenye ulemavu wa ngozi wapo 16,477 (0.04), wasioona  848,530 (1.19).

Amebainisha kuwa wasiosikia wapo  425,322 (0.97), wasioweza kutembea  525,019 (1.19), wanaopoteza kumbukumbu ni 401,931 (0.91).

Amesema idadi ya watu ambao hawawezi kabisa  kujihudumia ni  324,725 (0.74), ulemavu mwingine ni 99,798 (0.23).

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Khadija Nassiri Ali ambaye alitaka kujua Serikali kama inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu waliokuwa nao.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )