Tuesday, April 3, 2018

Aunty Ezekiel Ajibu Tuhuma za Kuazima Nguo kwa Wema Sepetu

Mwanadada Aunty Ezekiel amefunguka na kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili kuhusu tabia yake ya kuazima nguo kwa rafiki yake wa karibu Wema sepetu , tuhuma ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao kila kukicha.

Aunty Ezekiel  amesema kuwa nguo wanayosema ameazima zilishonwa mbli na yeye ndiye  aliyekuwa wakwanza  kuvaa nguo hiyo lakini anashangaa sana watu wanapokuja na kumtuhumu kuhusu swala hilo.

Hata hivyo Aunty anasema kuwa bado kwao sio shida kuvaliana nguo kwa sababu ni marafiki hivyo ni swala la kawaida.

"Kwanza kuazima nguo sio shida kwetu kwa sababu ni rafiki yangu lakini cha ajabu ni kwamba nguo wanayoizungumzia wao zimefanana wala hakuna aliyenda kugonga hodi kwa mwenzake."-Alijibu Aunty

Wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa ingawa hapo katikati walikuwa wakionekana kutokuwa pamoja lakini sasa ivi mapenzi yamerudi na kuwa mapya kabisa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )