Wednesday, April 25, 2018

Bashe Ahoji Ahadi Ya Rais Magufuli Kufufua Skimu Ya Umwagiliaji

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ameibana Serikali akiitaka itoe majibu kuhusiana na ahadi ya Rais John Magufuli mwaka 2015 ya kufufua Skimu ya Umwagiliaji katika kijiji cha Idudumo Wilayani Nzega.

Akiuliza swali bungeni leo Aprili 25, Bashe amedai kwamba mwaka 2015 wakati wa kampeni, Rais Magufuli aliahidi kuifufua Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Idudumo Wilayani Nzega.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema miradi ya utekelezaji inategemea na upatikaji wa fedha na ikipatikana itatekelezwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )