Tuesday, April 10, 2018

Chanjo Saratani Ya Kizazi Yazinduliwa Rasmi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti na ya mlango wa kizazi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi mkoani Dar es Salaam ambapo hafla ya uzinduzi zilifanyika kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, wilaya ya Temeke.

Makamu wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika

“ Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu. Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo.” Alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.

Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ni walengwa wa kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi  kwa mwaka huu 2018 ambapo jumla ya wasichana 6,16,734.

Makamu wa Rais ambaye aliwaeleza wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi kuwa anaunga mkono uwepo wa chanjo hiyo huku akitoa sababu mbili moja ikiwa ni kulinda jeshi la wanawake nchini Tanzania kwani wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao kwa sababu ya Saratani na sababu ya pili ni kwamba Mama yake Mzazi alifariki kwa kansa hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Wakati huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania imeandika historia nyingine katika sekta ya afya kwa kuzindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa Kizazi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )