Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 28, 2018

Familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zaanza kupata huduma

Zaidi ya familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zimepatanishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda.

Hayo yamebainishwa jana Aprili 27 na Makonda wakati akitoa majumuisho ya zoezi la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na wenza wao wakiwa na watoto.

Kadhalika Makonda, hakuacha kuwashukuru waandishi wa habari kwa kufanya kazi kubwa katika kuhabarisha umma kuhusu kampeni yake.

“Kwanza niwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri mliyofanya, lakini pia niwashukuru wote walionitukana kwa kuanzisha zoezi hili wakiwamo wabunge,"alisema.

Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwani  familia 208 zimeanza kupata huduma kutoka kwa baba zao.

Kadhalika amesema, kati ya watu 17,000 waliofika ofisini kwake, 90 wamefanikiwa kupimwa uhalali wa baba kwa mtoto ( DNA) na watoto 2971 wakifanikiwa kupata  bima ya afya.

"Tumeunda tume ya watu 15 watakaofuatilia kwa kina matatizo ya kiutawala katika kushughulikia masuala  yanayohusu jamii kwani imeonekana kuna shida kubwa kwa watu wanaoshughulika na ustawi wa jamii," alisema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )