Tuesday, April 17, 2018

Jacqueline Wolper aeleza ukweli kuhusu kutoifagilia WCB

Wiki iliyopita yalisambaa baadhi ya maneno yakisema kuwa Wolper amesema kuwa yeye sio shabiki wa WCB bali shabiki wa Diamond Platinumz tu, hii ikimaanisha kuwa hana mapenzi na wasanii wengine wa wcb zaidi ya bosi wa lebel hiyo.

Hata hivyo  Wolper amefunguka na kukanusha kuhusu maneno hayo na kusema kuwa watu waliomsikia walimuelewa vibaya kwa sababu si hivyo ambavyo wamefikiria ndivyo alivyomaanisha.

Wolper anasema kuwa kwa mtu anaelewa mahusianao yake na WCB hawezi kutilia mashaka swala kama hilo au kufuatilia kwa undani maneno hayo.

"Mtu akisikiliza kauli kama hiyo na ananijua mimi lazima atashangaa, mimi sio shabiki wa WCB, how? mimi nilijibu kutokana na swali nililokuwa nimeulizwa siku ile.kwaio watu wenye akili zao na wanaonielewa hawawezi kufatilia hivyo vitu."-Alisema Wolper.

Hata hivyo hivi karibuni Wolper alisema kuwa anaacha kumsapoti msanii Harmonize ambae alikuwa mpenzi wake hapo zamani kutokana na wivu alio nao mpenzi mpya wa msanii huyo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )