Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, April 27, 2018

John Heche Awatuhumu Polisi Kumchoma Visu Mdogo wake Hadi Kifo

Mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche anayejulikana kwa jina la Suguta, ameuawa kwa kuchomwa kisu.

Kwa mujibu wa John Heche mdogo wake amechomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari Tarime, huku akiwa na pingu mikononi, waliomkamata baada ya kumkuta bar akinywa pombe.

"Ni kweli kwamba mdogo wangu ameuawa na polisi, na ameuawa akiwa mikononi mwa polisi, jana usiku polisi walimkamata akiwa kwenye bar alikuwa na wenzake wanakunywa pombe, sasa wakamkamata, wameenda naye mpaka kituo cha polisi akiwa mzima wamemfunga pingu, askari mmoja akatoa kisu akamchoma eneo la mgongo kikaenda mpaka kikagusa chembe ya moyo, wamemchoma kisu akiwa wamemfunga pingu tena akiwa kituo cha polisi", amesema John Heche.

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Sirari wamejikusanya kituo hicho cha polisi kutaka maelezo zaidi

Kamanda wa Polisi Tarime hakupatikana kuongelea tukio hilo
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )