Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 26, 2018

Kandoro alazwa hospitali ya Benjamin Mkapa.....Waziri Mkuu Amjulia Hali

adv1
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Bw. Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
 
Akiwa hospitalini hapo jana (Jumatano, Aprili 25, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Bw. Kandoro na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri.

Pia Waziri Mkuu amemjulia hali Mbunge wa Viti Malumu (CUF) Bi. Shamsiha Azizi Mtambo ambaye amelazwa katika ya Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU)kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wake, Bw. Kandoro alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali, pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyokwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )