Thursday, April 26, 2018

Linah: Wasanii wa Kike Inabidi Tubadilike

Msanii mkongwe wa Bongo fleva nchini amefunguka na kuwaambia wasanii wa kike kuwa ili kuendelea kimuziki inabidi wabadilike na kukubali changamoto ili kuweza kuendelea.

Linah anasema kuwa wasanii wengi wa kike wamekuwa na tabia ya kuogopa kuthubutu au kuwa na aibu ya kufanya kitu flani kwa kuhofia kuangaliwa wa jamii au watu wanaomzunguka lakini ili kufanikiwa ni lazima kujitoa na kuji-brand ili kufanikiwa.

Akiongeana na Clouds Tv, Linah anasema kuwa wasanii wengine wa kike wamekuwa wakitaka kukaa wao katika nafasi hizo, wamekuwa wanaoneana wivu  kwa kushindwa kuwavuta au kuwaachia na wasichana wengine kuwa pale walipo wao.

Linah anasema kuwa wasanii wa kike inabidi waige mfano wa wasanii wakubwa wa kike kutoka nje , hakuna madaraja ya msanii mkubwa wa kike kuliko mwingine na hiyo yote ni kwa sababu wamekuwa wakisaidiana na  kuvutana kutoka chini.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )