Monday, April 2, 2018

Makonda 'Awashitaki' Kwa Rais Magufuli Wanaoingia Dar na Kutoa Matamko ya Kichochezi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewashtaki kwa Rais Magufuli baadhi ya watu (hajawataja kwa majina) kwa kudai kuwa wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi.

Mh. Makonda amewasilisha mashtaka hayo kwa Rais leo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la  ujenzi mradi wa kuongozea ndege katika vituo vinne hapa nchini.

Mh. Makonda amemuambia Rais Magufuli kwamba kuna watu wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi hivyo yeye kama kiongozi wa mkoa wanajaribu kuangalia utaratibu mzuri wa kisheria watolee matamko katika mikoa yao.

Aidha amesema kwamba "Mh. Rais Tumesikia sikia huko kwingine ila sisi kwetu hakuna waraka. Hakuna waraka popote pale ulipopita. Watu wamemwabudu bwana na mwokozi wao na Tumeungama dhambi zetu kupitia kufa kwake msalabani, tumefufuka naye na tunaendelea kufanya kazi kikamilifu".

Mbali na hayo Mku huyo wa Mkoa ameweka wazi kwamba wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wamesherehekea sikukuu ya Pasaka salama salimini kwani wananchi wametambua thamani ya amani.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )