Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 14, 2018

Makonda: Sina mpango wa Kugombea Urais...Lengo Langu ni Kumsaidia Magufuli

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hana mpango wa kuwa Rais ila anapenda kumsaidia Rais John Magufuli katika utekelezaji wa shughuli zake.

Makonda ameyasema hayo leo alipoulizwa na mwandishi wa Azam TV Baruan Muhuza wakati wa mahojiano yake akielezea tathmini ya siku tano za kusikiliza malalamiko ya wanawake waliotelekezwa na wenza wao.

Muhuza aliuliza: “Hao wote uliowasaidia wanakuona shujaa na mtu wao wa muhimu sana, unatamani kuwa rais wa nchi hii siku moja."

Makonda amejibu,“Hapana ila natamani kumsaidia Rais Magufuli atimize azma yake kwa wananchi hasa kwa malengo aliyonipa kwa mkoa wa Dar, hiyo ndiyo shauku yangu."

Kuhusu madai ya kuwachafua watu maarufu kupitia zoezi hilo amesema, "Huchafuliwi kwa kuwa una mtoto, matendo yako uliyoyafanya ndiyo yanayokuchafua,"

"Si kweli kwamba eti nililenga kuwachafua wanasiasa ndiyo sababu kuna DNA. Kama kuna mtu anafikiri ni zoezi la mtu fulani anakosea, namna pekee ya kuepuka kuitwa kwa RC mtafute mtoto wako umlee,"

Amesema shauku yetu kubwa ni kuona kila mtoto anapata haki yake.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )