Thursday, April 26, 2018

Mbunge Azifananisha Ndege za ATCL Na Daladala

Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amesema ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kutoa huduma za usafiri wa anga asubuhi hadi jioni na kusitishwa usiku hakiwezi kulinufaisha shirika hilo, huku akifananisha kitendo hicho na huduma za usafiri wa daladala.

Akizungumza bungeni Aprili 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, Bobali alisema hakuna anayepinga shirika hilo kufufuliwa lakini tatizo ni uamuzi wa Serikali kununua ndege bila kuboresha miundombinu na kuwa na mipango endelevu.

“Tunapaswa  tuelewane hakuna anayekataa wala kupinga ATCL kufufuliwa. Tunachopenda kushauri ni namna na njia inayotumika kulifufua shirika. Mawaziri mpo hapa mnasoma ripoti mbalimbali za mashirika ya anga ya kimataifa na mnajua nini kinaendelea kwenye mashirika ya ndege mengine,” alisema.

“Kwa sasa takwimu zilizopo, kwa mwaka mmoja mashirika ya ndege duniani yanapata hasara ya Dola 8 bilioni za Marekani, kwa Afrika pekee mwaka uliopita mashirika ya ndege yalipata hasara ya Dola 600 milioni za Marekani. Ikiwa hali ndio hii tukienda kuifufua ATCL lazima tuwe na tahadhali.”

Alisema katika mjadala huo, baadhi ya wabunge wamehoji kitendo cha ndege za ATCL kutoa huduma, huku viwanja vya ndege nchini vikiwa vibovu na hakuna usafiri wa usiku wa ndege.

“Wakati tunanunua ndege tulijua tunasafiri nje ya nchi, lakini najua kusudio la kununua ndege ni zitumike ndani, kwanini zaidi ya viwanja vya ndege asilimia 70 nchini havina taa?” alihoji.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )