Tuesday, April 10, 2018

Mke wa 8 wa Mfalme Mswati III, Senteni Masango amejiua kwa kunywa vidonge

Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki dunia akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita.

Vyombo vya habari nchini Swaziland vimeeleza kuwa Bi. Masango alitumia dawa aina ya AMITRIPTYLINE kupita kiasi (Overdose) kitu ambacho kimepelekea mwanamke huyo kupoteza masiha, hii ni baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Face 2 Face umeeleza kuwa Bi. Masango alichukua uamuzi huo wa kujiua Ijumaa ya Aprili 07 ya wiki iliyopita, Baada ya mumewe kumkataza kuhudhuria kwenye mazishi ya dada yake yaliyofanyika Jumapili ya Aprili 01, 2018.

Kufuatia tukio hilo, tayari serikali nchini Swaziland kupitia kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Dkt. Sibusiso Dlamini imetuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Mfalme Mswati (III).

Bi. Masango aliolewa na Mswati (III) mwaka 1999 na ameacha watoto wawili wa kike na leo Aprili 10, 2018 mwili wake unatarajiwa kuzikwa kwa heshima nchini humo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )