Tuesday, April 3, 2018

Rais Magufuli aitaka Tanesco kupunguza bei ya umeme

Rais John Magufuli amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuanza kufikiria kupunguza bei ya umeme kwani nchi inatarajia kuwa na umeme mwingi.

Rais ameyasema hayo leo Aprili 3, wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi awamu ya pili.

Amesema miradi yote ya umeme ukijumlisha na wa Stiegler Gauge itafikia megawati 5000 hivyo wataibana  Wizara ya Nishati ianze kufikiria kupunguza bei ya umeme.

“Muanze kufikiria namna ya kushusha bei ya umeme, mmeanza vizuri muendelee na utaratibu huo.

“Nchi ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, maji , jua, upepo, makaa ya mawe, hata nyuklia, kwa sababu tunayo madini ya uranium yanayoweza kuzalisha umeme kwa nyuklia, kwa umeme wote huo hakuna haja ya kuwa na bei ya juu, ”amesema Magufuli.

Amefafanua kuwa anayetaka kuwekeza bila kukomoa aje, lakini siyo wawekezaji wababaishaji.

Ameeleza kuwa nchi itakuwa na umeme wa kutosha,  wa uhakika na kwa gharama nafuu.

Magufuli pia alizitaja sababu za bei ya nishati hiyo kuwa ya juu ni kutokana na umeme mwingi kuzalishwa kwa kutumia mafuta (dizeli), huku baadhi ya mikataba kuwa mibovu na ya ovyo.

Ameeleza takwimu zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/16 zinaonyesha asilimia 36.6 ya Watanzania ndiyo wameunganishiwa umeme.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )