Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, April 29, 2018

Rais Magufuli kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Iringa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Iringa kuanzia leo  tar 29 mwezi huu hadi tar 4 mwezi ujao.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa wanatarajia kumpokea rais Dkt. Magufuli leo  tar 29 mwezi huu.

Alisema kuwa mara baada ya kupokelewa Rais Dkt. Magufuli atazindua barabara ya kijiji cha Migori kwenda Fufu kupitia Iringa mjini.

“Siku ya Mei Mosi Rais Dkt. Magufuli atakuwa mgeni rasmi, ambapo kitaifa yatafanyika mkoani hapa ambapo kutakuwepo na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu, Spika wa bunge na viongozi wengine,”alisema Masenza

Mkuu huyo wa mkoa wa Iringa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi ambapo zimepangwa kufanyika mkoani humo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Rais Magufuli akiwa ziarani mkoani humo atazindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo vikiwemo viwanda.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )