Tuesday, April 17, 2018

Shamsa Ford: Diamond Endelea Kuwatumia Hao Wanawake Maana Hawajielewi, Lakini Kumbuka Kutumia Kondomu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford Amefunguka na kudai kuwa sio kweli kwamba Diamond anawadhalilisha wanawake ambao wanatoka nao kimapenzi kwa kusambaza video zao mtandaoni.

Diamond alizua gumzo hili siku ya jana bada ya video zake kusambaa mtandaoni akiwa na Hamisa Mobetto chumbani wakikumbatiana na wakati huo huo akiwa na binti wa kizungu wakiwa pamoja chumbani pia Wakila denda na uchafu mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Shamsa aliulizwa nini maoni yake juu ya jambo hilo na alifunguka na kumtaka Diamond aendelee kutoka na wanawake tofauti tofauti kwa kuwa hawajitambui huku amtahadharisha kutumia kondom ili kuepuka magonjwa na zinaa.

"Mwanaume hawezi kukufanya mwanamke ukawa chombo cha starehe ...inategemea mwenyewe na akili yako,kama unataka kuchezewa utachezewa kama unataka kuwa mwanamke wa muhimu kwake utakuwa inategemea mwenyewe unajiweka wapi 

"Kwa hiyo mimi siwezi kumlaumu Diamond kama anawatumia maana wenyewe ndio wameweka mazingira hayo kwa nini asitumie nafasi? Ila mimi namshauri Diamond awale tu hao wasichana ila akumbuke kutumia kondomu maana magonjwa mengi”.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )