Thursday, April 5, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Nane ( 48 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikawaomba wanipishe njia, na wakafanyahivyo hadi nikafika kwenye mlango, nikaanza kugongwa kwa nguvu ulu nikiliita jina la Rahma, gafla moshi mwingi ukaanza kutoka chini ya mlango, ulio anza kutupalia watu wote tuliopo kwenye eneo hili la mlango

ENDELEA
Moshi mwingi ukazidi kutoka ndani ya chumba alichopo mke wangu Rahma, ambaye hadi sasa hivi anapiga kekelele za kuomba msaada, nikajitaidi kuibana pumzi yangu, nisiendelee kuuvuta moshi unaotoka kwenye chumba alichopo Rahma na kuanza kuubamiza mlango kwa kutumia bega langu la mkono wangu wa kushoto, kwa nguvu zangu zote.Kelele za Rahma zikazidi kunichanganya kiasi cha kujikuta nikizidisha juhudi za kuuvunja mlango kwa kutumia nguvu zangu zote.

Wanaume wezangu wakaanza kunisaidia kufanya kitendo ninacho kifanya mimi, cha kumshukuru Mungu, mlango ukavunjika na sote tukajikuta tukianguka nao baada ya kuurukia kwa nguvu zetu zote, Moshi mwingi tukakumbana nao, ulio ambatana na moto mwingi, nikamshuhudia msichana aliyekuwa amepigwa na Rahma akipotelea kwenye moshi mwingi ndani ya chumba, wezangu hawakumuona zaidi yangu
Nikakimbilia sehemu alipo Rahma na kumkuta akiwa amelala chini, huku hajitambui,
“Rahma, Rahma”

Nilimuita ila hakuitika zaidi ya kuendelea kuyafumba macho yake, tukasaidiana na wezangu kumnyanyua Rahma na kumtoa nje kwa haraka na kuanza kumpa huduma ya kwanza, rahaya ya sherehe ikanipotea kabisa na kuwa ni majanga mengine ambayo sikuyatarajia kama yatatokea katika siku hii ya leo, watu wengine wakaendelea kuuzima moto uiopo ndani ya chumba ambao hadi sasa hivi chanzo chake ni nini.Hali ya Rahma ikazidi kuwa mbaya kwani mapigo yake moyo yamekuwa ya kuhesabika na ndani ya dakika moja yanaweza kupiga mara tano au saba, ni tofauti na mapigo yamoyo yanavyopaswa kupiga kwa binadamu wa kawaida.Jamaa mmoja akajitolea gari lake, tukamuingiza Rahma ndani ya gari na kumuwahisha katika hospitali ya mkoa ijulikanayo kwa jina la Bombo.Akili na mwili vyote vimechoka kwa muda mmoja, kila daktari ambaye anatoka kwenye chumba anacho ingizwa mke wangu sikusita kumzuia na kumuuliza hali ya Rahma inaendeleaje ila hawakunipa jibu la kueleweka

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )