Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, April 1, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Sita ( 46 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Siipendi siasa, na sidhani kama ninaweza kuwa mbunge”
“Je kuna ukweli wowote kwamba wewe umepandikizwa roho ya nyoka?”
Swali la muandishi huyu wa habari likanifanya niiname chini ya meza kwani nilijikuta nikikasirika sana jambo ambalo taratibu nikanza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wangu, ubaridi mkali ukaanza kunitawala, huku ukiambatana na mikono yangu kuanza kubadilika jambo lililo anza kuniogopesha

ENDELEA
Nikastukia nikifunikiwa na taulo mgongoni, kuangalia vizuri nikamkuta ni Rahma ndio amenifunika na taulo ambalo limelowana maji, kidogo nikaanza kujihisi vizuri hata ubaridi mkali na mabadiliko kwenye mikono yangu vikaanza kuputea taratibu hadi nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida
“Unajisikiaje mume wangu?”
Rahma aliniuliza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza sana, ambayo sio rahisi kwa mtu yoyote kusikia

“Nipo powa”
“Twende basi ukapumzike ndani”
“Sawa”
“Jamani wapendwa Mr kidogo hali yake sio nzuri sana, ninawaomba mummpe muda kidogo, na mahojiano yataendelea jioni kwenye tafrija ndogo niliyo waandaliaa”
Rahma alizungumza na waandishi wa habari, taratibu akaninyanyua kwenye kiti, tarataibu tukaanza kuelekea ndani, Rahma kwa utaratibu akanilaza kitandani na kuniwashia feni lililopo pembeni ya kitanda changu
“Eddy vumilia, mume wangu”
“Mbona imekuwa hivi, sielewi?”
“Mume wangu pumzika kwanza nitakujibu baadaye”
Rahma alianza kunibembeleza taratibu, akaniacha na kwenda nje kuendelea na maandalizi ya tafrija fupi aliyo iandaa, nikaanza hihisi harufu ya tofauti ndani ya chumba changu, na taratibu nikaanza kunyanyuka kitandani mwangu, huku nikiongozwa na pua zangu, kunusa ni wapi harufu hiyo inapo tokea.Nikaanza kusikia vikopo vya kuwekea ,afuta vilivyopo bafuni vikianguka,

“Ni nini?”
Nilijiuliza kwa maana ndani kwat hakuna panya wala paka anayeweza kufanya uharibifu kama huo.Nikaendelea kutembea kwa umakini hadi bafuni na kukuta vikopo vyote vya mafuta na sabuni zikiwa chini, harufu nayo sikuihisi ndani mwangu tena.Nikaanza kuokota kimoja baada ya kingine, nikiwa nimeinama nikastukia kuiona miguu ya mwanake nyuma yangu, kupitia kioo kilichopo mbele yangu ikiwa inavuja damu nyingi, nikasimama na kugeuka na kukutana na binti wa miaka kama kumi na nane akiwa anavuja damu mwili mzima
Macho yake ameyatoa kiasi kwamba anaonekana kubanwa na kitu kwenye koo lake,
“Ni…nisa..idie”
Alizingumza kwa shida sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeshangaa kwani sikujua ameingiaje ingiaje ndani kwet na istoshe sikujua ni kitu gani kilicho mpata
“Wewe ni nani?”
“Ni…saaa iii..dieee”
Aliendelelea kuzungumza kwa shida sana, nikajaribu kuuinua mkono wangu ili nimpe, nikajihisi uzito mkubwa sana kutoka kwenye mkono wangu

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )