Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, April 8, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Hamsini ( 50 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya
“Mambo Eddy”
Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu

ENDELEA
Jamaa akatoka kwenye droo ya kuhifadhia maiti na kusimama karibu yangu, mwili mzimwa ukaanza kunitetemeka kwa maana katika maisha yangu sijawahi kukutana na vihoja kama hivi japo kuna matukio mengi ya kutisha yalisha wahi kupita kipindi cha nyuma ila la mtu anaye fanana na mimi kwangu limekuwa ni laajabu sana
“Usishangae sana”

Alizungumza huku akielekea walipo simama dokakta na nesi, akawatazama mlinzi na nesi ambao wamepoteza fahamu kisha akaachia tabasamu pana kidogo
“Hawa nao kilicho waangusha ni nini?”
Swali lake hapakuwa na mtu aliye lijibu zaidi ya sisi sote kubaki kimya tukimtazama, akachuchumaa na kumshika mlizi kichwani, gafla mlinzi akaanza kutoa chafya zilizo pelekea akazinduka na kukaa kitako na macho ya mlinzi yakabaki  kuwa na mshanga kati yangu na Eddy mwenzangu.Macho yangu yakatua kwenye suruali ya dokta na kukuta ikiwa imelowa maeneo ya mbele, ikiashiria ameshindwa kuibana haja yake ndogo kutokana na woga wa kukutanan na jamaa.Akamshika nesi kama alivyo fanya kwa mlinzi na neshi fahamu zikamrejea na kuzinduka.

“Ninaamini nyinyi nyote mutakuwa munashangaa kwa nini mimi nipo hivi, jina langu ninaitwa Eddy ni pacha wa Eddy yule pale”
Eddy alizungumza huku akiwatazama manesi, akangeukia kisha akamshika bega dokata ambaye hadi sasa hivi mwili wake wote namtetemeka mithili ya mtu aliye pigwa shoti
“Mzee usiogope sana, mimi sio mtu mbaya, ila kazi yangu ni moja tu.Nimekuja kumsaidia Eddy katika swala zima la kumrudisha mke wake ambaye hajafa kama munafyo fikiria nyinyi, ndio maana kwenye droo muliyo muweka hamjamkuta”
“Amekwenda wapi?”
Nilimuuliza kwa kujiamini
“Eddy hilo swali nitakujibu baadaye na si mbele ya hawa watu”

 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )