Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 26, 2018

Wema Sepetu Agoma Kuigiza na Mama Yake Kanumba

adv1
Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.

Wema ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake ajiingize kwenye Bongo movie.

Wema alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:

"Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama Kanumba kuwa alipowenda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake aliishia kuchomeshwa mahindi:

"Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )