Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 14, 2018

Zitto ampa pole RC Gambo kufuatia kifo cha mama yake

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo baada ya kufiwa ya mama yake mzazi usiku wa kuamkia jana.

Zitto amesema kuwa anajua uchungu wa kupotelewa na mama huku akieleza kuwa hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.

"Pole sana kwa Msiba huu mkubwa ndugu Mrisho Gambo. Najua uchungu wa kupotelewa na mama. Hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi. Mola akupe subira wewe na ndugu zako. Inna lilah waina ilaih raajiun ameandika Zitto kwenye mitandao yake ya kijamii."-Zitto Kabwe
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )