Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, April 12, 2018

Zitto ataka Tamisemi imtafute mwenyekiti aliyetoweka

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue.

Amesema hayo bungeni leo Aprili 12, 2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, yenye wizara za Tamisemi; na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo, sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema.

Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya.

Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika.

“Familia imechukua hatua mbalimbali, imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao, hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,” alisema Zitto.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )