Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, May 15, 2018

Apandishwa Cheo Baada ya Ziara ya Kushtukiza ya Rais Magufuli

adv1
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA bandari ya Dar es Salaam Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili bandarini hapo ndani ya wiki hii.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo wakati alipokuwa anazungumza na  viongozi mbalimbali kwenye bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwenye bandari na kusema amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ben Usaje katika kusimamia maslahi ya nchi vizuri.

"Nawapongeza watu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi nzuri mnayoifanya,  Waziri wa Fedha kampeni tu huyu ukamishna kamili kwa sababu amesimamia haki halisi kwaajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, najua wanamchukia sana wengine wafanyabiashara lakini waache wakuchukie Mungu anakupenda na watanzania tutaendelea kukupenda kwa hiyo mka-confirm. Katibu Mkuu mkazungumze wote mumpe angalau ndani ya wiki hii msimcheleweshe", amesema Dkt. Magufuli.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli umekuja baada ya kumuuliza swali Kaimu Kamishna kuwa anafanya kazi gani TRA na ndipo alipotoa amri hiyo ya kupandishwa cheo haraka kutokana na kuwa ameweza kusimamia haki na maslahi kwa ufasaha.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )