Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, May 6, 2018

Binti abakwa na kuchomwa moto akiwa hai

adv1
Polisi wa India wamesema kwamba , msichana wa miaka 16 nchini humo amechomwa moto  akiwa hai baada ya wazazi wake kulalamika kwa wazee wa kijiji kuwa binti huyo amebakwa.

Inspekta wa Polisi, Shambhu Thakur alipozungumza na gazeti la Hindustan Times amesema kwamba watu 14 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo katika Jimbo la Mashariki mwa India Jharkhand.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, Polisi huyo amesema wazee wa kijiji waliamuru wanaotuhumiwa  kuhusika na ubakaji huo walipe faini ya Pauni 550 kama adhabu.

Watu hao walikasirishwa na uamuzi huo na kuamua kuwapiga wazazi wa msichana huyo kisha kumchoma moto binti yao.

''Watuhumiwa wawili waliwapiga wazazi kisha wakakimbilia kwenye nyumba yao wakiwa na washirika wao na kumchoma moto msichana,” Ofisa wa Polisi, Ashok Ram alisema.

Polisi wanasema binti alibakwa na wanaume wawili katika eneo lenye msitu karibu na kijiji cha Raja Kendua baada ya kutekwa akiwa peke yake nyumbani kwao baada ya wazazi wake kuelekea kwenye harusi.

Baada ya tukio hilo wazazi walikwenda kupeleka mashtaka kwa wazee wa kijiji kuwashtaki wabakaji.

Mabaraza ya kijiji hayana nguvu kubwa ya kisheria, hata hivyo yana ushawishi mkubwa kwenye sehemu nyingi ya vijiji vya nchini India katika kusuluhisha migogoro kuliko kutumia gharama nyingi kwenye mfumo wa mahakama.

Polisi katika jimbo hilo wamesema wamewakamata watu 14 kati ya 18 ambao watachunguzwa kutokana na madai ya ubakaji na uuaji.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )