Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, May 14, 2018

Kauli ya Steve Nyerere Baada ya Lulu Michael Kuachiwa Huru

Taarifa za muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael”Lulu” kuachiwa huru siku ya leo May 14,2018 zimewafurahisha wengi baada ya kubadilishiwa adhabu na kumalizia adhabu yake nje ya gereza.

Mchekeshaji Steve Nyerere ambaye pia ni msemaji mkuu katika kitengo cha waigizaji (Bongo Movie) ni mmoja wa watu waliofurahishwa na taarifa hizo na kuonesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa instagram.

“Lulu ni jambo la kushukuru sana kwani kila pito naamini Mungu supo pamoja nawe, nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kumshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa msamaha huu naamini umefanya jambo jema sana Rais wangu. Nipongeze mahakama pia na wadau wote mliokuwa mnamuombea mwenzetu kutoka familia njoo Lulu tujenge tasnia yetu sasa”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )