Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, May 15, 2018

Lulu Michael Keshaanza Kutumikia Kifungo chake cha Nje kwa Kufanya Usafi Wizarani ya Mambo ya Ndani

Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu ameanza kutumikia kifungo  chake cha nje kwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nzase amesema Lulu anaungana na wafungwa wengine 10 wanaofanya usafi wa mazingira wizarani hapo.

Amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa Taifa.

Ameongeza kuwa tayari msanii huyo alianza kutekeleza adhabu hiyo tangu jana na kwamba ataendelea mpaka atakapomaliza kifungo chake Novemba, mwaka huu.

“Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira,” amefafanua Nzase.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...