Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, May 10, 2018

Mahakama yapokea vielelezo kesi ya Nondo

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa, imepokea vielelezo vya kimtandao vilivyoletwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo.

Akizungumza Mahakamani hapo, leo Mei 10, Hakimu Mkazi, wa mahakama hiyo, John Mpitanjia amesema amepokea vielelezo hivyo baada ya kupitia sheria mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Mpitanjia amesema, mahakama inawajibu wa kupokea kila kielelezo kinachokuja mbele yake.

Baada ya uamuzi huo upande wa utetezi chini Wakili Chance Luoga uliridhia maamuzi hayo na kuomba kesi hiyo  iendelee tena Mei 14

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu,(TSN) anakabiliwa  anakabiliwa na mashtaka mawili shtaka la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )