Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, May 23, 2018

Msukuma: Profesa Lipumba na Sakaya ni Mabingwa wa Kuvuruga Vyama vya Siasa

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amefunguka na kudai kufarakana kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na CUF kimesababishwa na mzimu wa Profesa Lipumba na wala sio kitu kingine ambacho watu wanafikilia.

Musukuma ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na  EATV baada ya kuulizwa ni kiongozi gani wa upinzani anayemvutia.

"Mwanasiana wa upinzani anayenivutia ni Profesa Lipumba anajua hesabu za kuvuruga vyama nampenda sana, Lipumba yeye na Sakaya ni mabingwa wa kutibua siasa anajua kupiga hesabu za kuchekecha vyama, hata kufarakana kwa CHADEMA na CUF ni mzimu wa Lipumba huo", Musukuma.

Pamoja na hayo, Musukuma ameendelea kwa kusema "Lipumba nampenda kwa sababu ni mvurugaji wa hivi vyama vidogo vidogo, anaifanyia kazi nzuri sana CCM, yule ni 'master' wa kuvuruga".

Kwa upande mwingine, Joseph Msukuma amesema katika maisha yake anatamani awe fundi wa hesabu za siasa za kuvuruga vyama kama alivyo Prof. Lipumba.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )