Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, May 3, 2018

Ofisa Utumishi Asimamishwa Kwa Kukaidi Kuwarudisha Watumishi Waliokuwa na vyeti vya Darasa la 7

adv1
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Peter Nyalali, amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Utumishi wa halmasahauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 licha ya serikali kuagiza warejeshwe.

Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa kuanzia Mei Mosi, mwaka 2004, ambapo mara baada ya kauli hiyo Nyalali alimwagiza Dibogo kuwarudisha kazini watendaji hao 41 wa vijiji.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Ofisa huyo Utumishi anadaiwa kutotekeleza agizo hilo jambo lililomlazimu mkurugenzi kumsimamisha kazi.

Nao baadhi ya watumishi waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa miezi minane walitoa shukrani zao kwa serikali na kuahidi kuendelea kuwa wachapakazi.

Mei 2, mwaka 2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini na baadaye kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )