Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, May 31, 2018

PICHA: Kinana Akabidhi Ofisi Kwa Katibu Mpya wa CCM

adv1
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo Alhamisi Mei 31, 2018 amemkabidhi ofisi mrithi wake, Dk Bashiru Ally katika ofisi ndogo za chama hicho tawala, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Baada ya makabidhiano hayo, wawili hao waliingia katika kikao cha ndani na wafanyakazi wa chama hicho.

Dk Bashiru anakuwa Katibu Mkuu wa nane wa CCM baada ya kujiuzulu kwa Kinana aliyemuandikia barua mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli aridhie ombi lake hilo.

Mei 29, 2018 Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM na ambayo ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, ilimpitisha Dk Bashiru ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )