Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, May 15, 2018

Serikali yabanwa Bungeni migogoro ya wakulima na wafugaji

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeitaka Serikali kuwasilisha bungeni taarifa ya Tume iliyochunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji ili chombo hicho cha Dola kiweze kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba.

Akisoma taarifa ya kamati hiyo leo bungeni Mei 15, 2018, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Christine Ishengoma amesema migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ina athuri uzalishaji  katika sekta ya kilimo.

Amesema migogoro hiyo imesababisha hofu, uvunjifu wa amani, vifo na uharibifu wa mali na mazingira.

Dk Ishengoma amesema uchambuzi wa kamati umebaini migogoro ya matumizi ya ardhi ni mtambuka hivyo suluhu yake inaweza kupatikana kupitia jitihada za pamoja miongoni mwa sekta husika.

“Kwa kutambua hivyo na kuzingatia malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wabunge bungeni ambao kimsingi ndio wawakilishi wa wananchi, yalipelekea Serikali kuunda Tume inayohusisha wizara tano zinazohusika na ardhi,” amesema Dk Ishengoma.

“Kamati inashauri ni vyema taarifa ya Tume hiyo ikawasilishwa bungeni ili Bunge liweze kutekeleza wajibu wake wa kuishauri Serikali.”

Dk Ishongoma amesema Serikali iongeze kasi ya kutekeleza kwa vitendo Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999, pamoja na kuhuisha sheria nyingine zinazosimamia matumizi, umiliki, uhifadhi ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu ardhi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )