Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, May 15, 2018

Wanafunzi wazuiwa kwenda shule baada ya mto kujaa maji

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoga, Kitongoji cha Tambani wilayani Mkuranga, Amiri Mbamba ameagiza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaolazimika kuvuka Mto Kizinga, kutokwenda shule baada ya mto huo kujaa.

Mbamba alitoa tangazo hilo jana jioni Mei 14, 2018 kwa kupita katika nyumba za eneo hilo na kuwasihi wazazi wasiwaruhusu watoto wao kutoka majumbani kwa ajili ya usalama wao.

Mto Mzinga ulianza kujaa maji jana saa tatu asubuhi jambo lililowalazimu wavushaji eneo la Bonde la Mkoga kusitisha kazi hiyo.

Hata hivyo, hali ya kujaa maji iliongezeka jana Jumatatu jioni na kusababisha sehemu ya daraja iliyokuwa ikitumika kufunikwa na maji hayo.

Tangazo hilo pia liliwagusa wavushaji ambao wametakiwa kutovusha mwanafunzi yeyote hadi maji yatakapopungua.

Watu wazima ambao walikuwa wanavuka kwenye mitumbwi walilazimika kulipa gharama ya Sh1,500 hadi Sh2,000.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )