Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, May 3, 2018

Waziri Mkuu amkingia kifua Rais Magufuli

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maamuzi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria iliyokiukwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 3, 2018) Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Bibi Felista Bura ambapo alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuupandisha hadhi mji wa Dodoma.

"Rais Dkt. Magufuli hakukiuka sheria kwa sababu ana mamlaka kwa mujibu wa katiba ibara 2 na sheria ya Mamlaka ya serikali za Mitaa sura ya 288 kupandisha hadhi mji au eneo lolote kadiri ya mahitaji yatakavyohitajika. Hata kitendo cha Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali pamoja na upatikanaji wa miundombinu muhimu kama ya afya, maji, umeme, barabara na kuendelea kukua kwa ukusanyaji mapato ni vigezo tosha vya kuufanya mji wa Dodoma kuwa Jiji", amesema Waziri Majaliwa.

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema "Dodoma inajitosheleza kwa mahitaji mengi ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali muhimu kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, vyuo vikuu zaidi ya vitano, Ofisi ya UN, hivyo nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kwani unaleta tija kwa wananchi. Nashauri jambo hili lipongezwe badala ya kubezwa".

Aprili 26, 2018 Rais Dkt. Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )