Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 12, 2018

Amber Lulu Amuonea Huruma Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago ‘video vixen’ Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amemfungukia mzazi mwenziye na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobeto kuwa, anamsikitikia kipindi anachopitia kutokana na kuendelea kuandamwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizingumza na GPL, Amber alisema kwamba anaamini Mungu atampigania Mobeto kwa kuwa yanayo-mtokea ni mapito yapo kwa muda tu ikifika wakati kila kitu kitakuwa sawa na furaha yake itarudi kama zamani.

“Mimi namuamini sana Mobeto na ninajua kwamba ni mwanamke anayejiamini kwa kila kitu, kwa hivyo hili lililomtokea ni changamoto tu katika maisha niseme tu kwamba yeye aendelee na biashara zake kwa nguvu zote na kufanya kazi ili aweze kulea familia yake, achukulie hii ndio changamoto ya yeye kukaza buti na kutafuta mkwanja kwa juhudi zote, mwanaume kama anampenda atarudi tu,” alisema Amber.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )