Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 18, 2018

Askofu wa Kanisa la Agape Sanctuary International Akamatwa Kwa Utapeli wa Milioni 63

adv1
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Askofu Martin Gwila wa Kanisa la Agape Sanctuary International kwa tuhuma za utapeli wa kiasi cha zaidi ya milioni 63

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema kiasi hicho cha fedha alikipata baada ya kuwadanganya watu mbalimbali kuwa atawapa ajira kupitia kanisa lake.

Pia anadaiwa kuwalaghai waumini akiwataka watoe fedha ili wasajiliwe na alitoza viwango tofauti vya fedha.

“Askofu huyo alikamatwa mwishoni  mwa  wiki jijini Dodoma na alipokea fedha hizo pasipo kutoa ajira yoyote huku akitoa vitisho kwa waliotoa fedha hizo,” alisema

Kamanda Muroto  amesema kuwa kanisa hilo ambalo makao yake makuu yapo Arusha halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kama kanisa bali aliisajili Agape Sanctuary kama kampuni binafsi.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakani muda wowote kuanzia sasa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )