Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 25, 2018

Atiwa Mbaroni kwa kuuza sambusa za Paka

adv1
Mwanaume mmoja nchini Kenya amenusurika kuuawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya Wananchi hao kugundua kuwa Mwanaume huyo amekuwa akiwaauzia sambusa za nyama ya Paka kwa miaka 7.

Mr. James Mukangi anadaiwa kuwauzia wauzaji wa sambusa nyama hiyo ya Paka ikiwa na yeye pia hutengeneza sambusa hizo za nyama ya Paka huku wateja wake wengine akiwauzia nyama hiyo ya paka.

Mwanaume huyo anadaiwa kufanya biashara hiyo haramu kwa kipindi cha miaka 7 na anakadiriwa kuwa ameuza zaidi ya Paka 1000 toka mwaka 2012 huku akipata zaidi ya 11,000 za Kitanzania kwa kila Paka.

Pia Mukangi aliwaeleza Waandishi wa Habari kuwa aliamua kufanya biashara hiyo baada ya kuona kuna pengo sokoni la nyama hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za Kenya Paka sio mfugo anayeruhusiwa kutumika kama kitoweo nchini humo.

Aidha jamaa huyo alikamatwa na Wananchi mjini Nakuru nchini Kenya alipokuwa akiwachuna ngozi Paka na ndipo Wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo kabla ya Polisi kuja na kumuokoa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )